Monday, February 25, 2013

IJUE FIRST Q...

Kuna wengi wanafanya mengi kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Tumeona waimbaji, wahubiri na wengine wengi lakini hii ni ya kipekee na kimsingi mimi binafsi sijawahi ona labda niseme kwa hapa Tanzania huwa naona watu wanajipanga na kuandaa 'show' ya kucheza kucheza kwenye masherehe na sehemu mbali mbali.

Kitu ninachofahamu kwamba hivyo vipaji vinatoka kwa Mungu! Na ni dhahiri kuwa kile alichokupa Mungu, anatamani ukitumie kwa utukufu wake. 

1st Q ni kundi linalohusisha vijana mbali mbali ambao kwa sasa wanashugulika na swala zima la kucheza kwa kumtukuza Mungu. Biblia inasema "Msifuni kwa matari na kucheza..." Zaburi 150:4 (Praise Him with a timbrel and dancing, .... Psalms 150:4).

Niliongea na muanzilishi (mbeba maono) wa kundi zima la 1st Q ambaye ni Grace Lifard, na haya ndiyo niliyotamani kujua toka kwake ili nawe upate habari.

Kwanza kabisa, kutaka kujua kiundani 1st Q  ni nini...
Alisema kuwa 1st Q ni 'organization' ambayo imeanza rasmi kazi zake mwezi wa 4 mwaka 2012 na kwa sasa inajihusisha sana na kucheza japo mbeleni matazamio ni kuongeza mambo mengine mengi ambayo yatawawezesha watu kutumia vipaji vyao kwa ajili ya kumtukuza Mungu kama ambavyo kwa sasa inafanyika kwa kucheza.

Kwa nini jina 1st Q?
1st Q inamaanisha first quadrant. Ni jina ambalo limetokana na msingi wa Hisabati. katika majira ya nukta, kuna x na y ambapo quadrant ya kwanza ina namba ambazo ni chanya zote na sababu sis tunaamini kwamba Mungu anafanya kazi na wampendao katika kuwapatia mema (Warumi 8:28), kila kitu kitakuwa sawa.

Sababu ya kuwepo kwa 1st Q...
Kuna sababu nyingi ikiwemo
  • Kuwapa watu nafasi ya kutumia vipaji vyao kumsifu Mungu
  • Kuto kumpa nafasi shetani kutumia vipaji ambavyo Mungu ameweka ndani yetu, na kwa sehemu kanisa limevisahau
  • Kuinua "gospel entertainment industry", watu waweze kufurahi wakiwa katika uwepo wa Mungu


Tangu kuanzishwa kwa 
1st Q  members waliopo ni Grace Lifard, Belinda Lifard, Mgeni Kabisama, Lamlo Kabisama, Jabz Sam, Hope Ndalima, Tenes Johanson, Lightness Wilson, Lisa Baraba.  Hawa ni kwa upande wa dancing.
Members wengine ni kama Daniel Mganga (mshauri), Agnes Lifard (mlezi msaidizi), Doreen, Mama Mlawa, Pastor Lucy Wilson, Lusajo Mwamakula, Mwl. Patrick.


Jinsi ya kuwapata 1st Q
wasiliana nao kupitia namba 0719 86 87 02
au kwa email lifarda1@gmail.com
pia unaweza kuwaona katika facebook kupitia page yao https://www.facebook.com/pages/1st-Q

Mungu akubariki kwa utukufu wa Jina la YESU!!! AMEN!!!