Pasaka imekaribia, leo ikiwa Ijumaa kuu tunakumbuka kuteswa kwa Bwana wetu Yesu Kristo kwa ajili ya dhambi zetu. Wengi wanapanga mengi ili tu siku ya pasaka iwe ya furaha. Tutaandaa, nguo, vyakula, tutajiandaa kwa ibada, wenye kusafiri kujumuika na ndugu zao au marafiki hufanya hivyo pia. Pia wapo wengine wanajipanga kwa mambo hata yasiyo husiana na dhima nzima ya sikukuu hii.
Sidhani kama nitakuwa nakosea nikisema kuwa sikukuu hii imewekwa kwa ajili ya kukumbuka swala zima la ukombozi. Neno la Mungu linatuammbia mara kwa mara kuhusiana na habari hizi lakini kuadhimisha siku hii iwe ni alama kwetu kuona uhalisia wa sisi kukombolewa na Yesu.
Kaa tayari, katika kuadhimisha tukio zima la ukombozi alioufanya Bwana Yesu. Isiwe kufurahi tu kwa kula na kunywa bali ifanye siku hii kuwa halisi na iweke alama katika maisha yako ya wokovu!
Fanya kama haijawahi kutokea pasaka hapo kabla katika maisha yako. Ifanye iwe siku ya pekee kwasababu ndivyo ilivyo, kila pasaka ni ya tofauti na Mungu ataachilia kitu kipya katika maisha yako.
Mungu akubariki na nakutakia pasaka njema!!!